Leviticus 8:1-12

Kuwekwa Wakfu Kwa Aroni Na Wanawe

(Kutoka 29:1-37)

1 Bwana akamwambia Mose, 2 a“Waletee Aroni na wanawe mavazi yao, mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili na kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu. 3 bKisha kusanya mkutano wote kwenye ingilio la Hema la Kukutania.” 4Mose akafanya kama Bwana alivyomwagiza, na mkutano ukakusanyika kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

5Mose akaliambia kusanyiko, “Hili ndilo Bwana ameagiza lifanyike.” 6 cKisha Mose akamleta Aroni na wanawe mbele, akawaosha kwa maji. 7 dAkamvika Aroni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi. 8 eAkaweka kifuko cha kifuani juu yake, na kuweka Urimu na Thumimu
Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
kwenye hicho kifuko.
9 gKisha akamvika Aroni kilemba kichwani pake, akaweka lile bamba la dhahabu, yaani ile taji takatifu, upande wa mbele wa kilemba, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

10 hNdipo Mose akachukua mafuta ya upako na kuipaka maskani na kila kitu kilichokuwamo ndani yake, kisha akaviweka wakfu. 11 iAkanyunyiza baadhi ya mafuta juu ya madhabahu mara saba, akaipaka madhabahu mafuta na vyombo vyake vyote pamoja na sinia na kinara chake, ili kuviweka wakfu. 12 jAkamimina sehemu ya hayo mafuta ya upako kichwani mwa Aroni, akamtia mafuta ili kumweka wakfu.
Copyright information for SwhNEN